Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) linawajulisha Waislamu na wananchi wote kwa ujumla kuwa Sikukuu ya Eid El-Fitri itakuwa tarehe 21/04/2023 au 22/04/2023 In shaa Allah. Sherehe za Eid El-Fitri kitaifa kwa mwaka huu zitafanyika Mkoa wa Dar es Salaam.
Swala ya Eid itaswaliwa katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI BAKWATA Makao Makuu Kinondoni kuanzia saa 1.30 asubuhi na kufuatiwa na Baraza la Eid litakalofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere kuanzia saa 8.30 mchana In shaa Allah.
Kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania Mh. Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Dr. Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally Mbwana anawatakia Waislamu na wananchi wote maandalizi mema ya Sikukuu hiyo. Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.