ZINAZOVUMA:

Mabaki ya kale ya mbao yagunduliwa Kalambo

Mabaki ya kale yaliyotengenezwa kwa mbao yamegunduliwa mpakani mwa Zambia...
Mabaki ya muundo wa kali yaliyogunduliwa karibu na Mto Kalambo.

Share na:

Mabaki ya kale ya muundo wa mbao. yamegundulika mpakani mwa Zambia na Tanzania.

Mabaki hayo yenye ishara ya kukatwa na kukwaruzwa kwa zana za mawe, yamepatikana pembezoni mwa Mto Kalambo.

Inaaminika kuwa mabaki ya kale hayo ni sehemu ya magogo mawili yaliyotumika, na watu wa kale walioishi pembezoni mwa Mto Kalambo nchi Zambia.

Profesa Larry Barham ni mmoja wa wanaakiolojia waliogundua mabaki hayo.

Profesa Larry alisema kuwa, “Mbao na jiwe zinaonyesha kiwango cha juu cha ustadi, teknolojia na mpangilio”.

Kauli hii ya Prof. Barham aliitoa baada ya kuona jinsi mbao hiyo ilivyokaa kwa ustadi a sehemu ya jiwe.

Muundo huo uliotengenezwa kwa mbao na mawe, unaohisiwa kuwa ni jukwaa mithili ya daraja au sehemu ya kuhifadhia chakula.

Mabaki yamepiwa na kuonekana ni ya miaka laki 476, huku wakiihusisha na stadi za Homo heidelbergensis badala ya Homo sapiens waliokuja baadae.

Mabaki hayo yangweza kuoza na kuisha, kama yasingefunikwa na maji kuzuia hewa ya Oksijeni kufikia mabaki hayo.

Mbali na muundo huo mithili ya jukwaa, pia walipata mabaki mengine mbalimbali kutoka katika eneo hilo.

Juhudi za kutafuta mabaki maeneo hayo zilianza mwaka 2006, na walitarajia wataendelea walipoishia ila wakakuta machimbo yamejaa maji ikabidi wahame.

Mto Kalambo unatokea Zambia na kupita katika maporomoko ya Kalambo, kasha maji yake yanaingia katika Ziwa Victoria Kusini Magharibi mwa Tanania.

Na mabaki hayo yamepatikana katika maeneo tofauti tofauti katika mto huo.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya