ZINAZOVUMA:

Ajali nyingne, ziwa Victoria

Watu 20 wamepoteza maisha baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama...

Share na:

Watu 20 wamethibitishwa kufariki baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama maji kwenye Ziwa Victoria nchini Uganda, ajali iliyotokea maajira ya saa tano asubuhi ya leo.

Boti hiyo ilikuwa na watu 34 na ilikuwa ikitokea kisiwa cha Bukasa kuelekea Entebbe, ambapo polisi wanasema watu 9 wameokolewa, huku chanzo cha ajali hiyo kimethibitishwa kuwa ni upakiaji kupita kiasi na hali mbaya ya hewa

Kwa mujibu wa maofisa wa polisi nchini humo, boti hiyo ambayo ilikuwa imejaa kupita kiasi, ilikuwa pia imebeba magunia ya mkaa, chakula na bidhaa nyengine.

Hii ni ajali ya pili ndani ya wiki moja kutokea katika ziwa Victoria, ya kwanza ikiwa ni Ile ya Mwanza Tanzania iliyohusisha vifo vya watu 13.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya