ZINAZOVUMA:

M.A.T yatoa tamko madaktari 162 waliofutiwa Shahada zao.

Chama cha madaktari Tanzania kimepokea kwa masikitiko taarifa ya wahitimu...

Share na:

Chama cha Madaktari Tanzania kimetoa tamko kuhusu wahitimu wa udaktari 162 waliofutiwa matokeo na Baraza la seneti la Chuo kikuu cha mtakatifu Augustine SAUT.

Ikumbukwe hivi karibuni kulitolewa Tangazo kupitia vyombo vya habari na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii likihusu kufutwa kwa vyeti vya uhitimu vya madakatari 162 waliosoma katika chuo kikuu kishiriki cha afya na sayansi shirikishi cha Mtakatifu Francis (St. Francis University College of Health and Allied Science – SFUCHAS) kipindi cha mwaka 2015 mpaka 2019.

Chama cha Madaktari (MAT) kimepokea kwa mshituko na masikitiko makubwa taarifa hiyo. Chama kimefuatilia kwa karibu sakata hili na kuja na ushauri kuhusu namna bora ya kulishugulikia ili kulinda hadhi na maadili katika tasnia ya udaktari.

Chama kimegundua uwepo wa dosari katika uwekaji wa alama za ufaulu tofauti na miongozo iliyopaswa kutumika kutoa alama husika wakati wakihitimu masomo yao.

Chama cha madaktari kinaona adhabu iliyotolewa na chuo tena kwa kujulisha umma ni ya kudhalilisha wahitimu hawa huku ikilinda hadhi ya wahusika wakuu.

Sintofahamu hii imewadhalilisha wahitimu hawa sana na kuwashushia heshima kwa jamii isitoshe, fani ya udaktari haina madaraja kama ilivyo kwa fani zingine hivyo pana uwezekano mkubwa tu kuwa baadhi ya walioorodheshwa kwenye tangazo la kufutiwa vyeti hawakuwahi hata kuchukua vyeti vya alama ya ufaulu.

Pamoja na miongozo mingine iliyotolewa na chama pia imelitaja Baraza la chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT SENATE) ifute tangazo lake la kufuta vyeti vya uhitimu (conferred degree) kwa wahitimu hawa wote na litoe nafasi kwa wahitimu kukutana na Braza la SENATE kwa ajili ya kurekebisha dosari zilizojitokeza.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya