ZINAZOVUMA:

Marekani na Urusi kubadilishana wafungwa

Urusi na Marekani zinajadiliana kuhusu kubadilishana wafungwa ambao kila nchi...

Share na:

Marekani na Urusi zinajadili uwezekano wa kubadilishana wafungwa ambao unaweza kumhusisha mwandishi wa gazeti la Wall Street Journal, Evan Gersh-kovich, ambaye anazuiliwa katika gereza la Moscow, kwa tuhuma za ujasusi ambazo alizakanusha.

Mfungwa wa pili ni raia wa Urusi ambae anazuiliwa Marekani kwa tuhuma za uhalifu wa mtandaoni.

Msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov aliwaambia waandishi wa habari kwamba maafisa wa Urusi na Marekani, wamejadiliana kuhusu kubadilishana wafungwa, hatua ambayo inaweza kuwahusisha Gersh-kovich, na Vladimir Dunaev, ambaye alihamishwa kutoka Korea Kusini, na yuko kizuizini katika jimbo la Ohio, nchini Marekani.

Siku ya Jumatatu, Marekani ilitoa idhini kwa Dunaev kuwasiliana na ubalozi wa Urusi, kwa mara ya kwanza tangu kukamatwa kwake mwaka wa 2021, wakati Lynne Tracy, balozi wa Marekani mjini Moscow, alipomtembelea Gersh-kovich, kwa mara ya pili tangu kukamatwa kwake, mwishoni mwa mwezi Machi.

Hakukuwa na dalili kwamba ubadilishanaji wa wafungwa hao ulikuwa karibu kufanyika, huku mahakama ya Urusi ikitoa uamuzi wiki iliyopita kwamba Gersh-kovich anaweza kuwekwa kizuizini hadi Agosti 30 na nchi hiyo, mara nyingi ikisema kwamba ubadilishanaji wowote, haungeweza kufanywa hadi uamuzi wa kesi hiyo, utolewe.

Tarehe ya kusikilizwa kwa kesi hiyo, bado haijatangazwa.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya