ZINAZOVUMA:

Israel imeua wahudumu wa afya zaidi ya 500

Share na:

Katika mashambulizi mbalimbali ya Israel dhidi ya ukanda wa Gaza, imekuwa sababu ya wafanyikazi zaidi ya 500 wa sekta ya afya kuuwawa tangu kuanza kwa mashambulizi hayo hadi leo.

Mashabulizi hayo yaliyoanza Oktoba 7 mwaka jana, ilionyesha ulimwengu tukio la kusikitisha kwa Wizara ya Afya ya Palestina kuzingirwa na vikosi vya Israel wakati dunia ikiadhimisha siku ya Kimataifa ya wauguzi.

Msemaji wa Hospitali ya Mashahidi wa Al Aqsa, Khalil al Daqran

Hapa Palestina na Gaza haswa, siku hii inapita huku wavamizi wa Israel wakiwa wameua wauguzi 138.

Siku ya Kimataifa ya Wauguzi mwaka huu ni ya kipekee, na ni haki yetu kuutaja mwaka huu kama Mwaka wa Uuguzi,” alisema msemaji wa wizara hiyo Khalil al-Daqran wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Kikao hicho na waandishi kiliandaliwa na wauguzi katika Mashahidi wa Al-Aqsa, Hospitali iliyopo katika mji wa Deir al-Balah katikati ya Ukanda wa Gaza.

“Wauguzi, wakunga na timu za matibabu ni sehemu muhimu ya muundo wa watu wa Palestina. Walikuwa mashahidi waliotekeleza jukumu lao la kitaifa na kibinadamu, kuokoa maisha ya waliojeruhiwa na wagonjwa,” alisema al-Daqran.

Al-Daqran alitoa wito kwa “jumuiya ya kimataifa na watu huru wa ulimwengu kuwalinda wafanyikazi wa matibabu na taasisi za afya na kuhalalisha mashambulizi dhidi yao.”

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya