ZINAZOVUMA:

Iraq imemfukuza Balozi wa Sweden nchini kwake

Iraq imemfukuza Balozi wa Sweden nchini kwake kufuatia maandamano ya...

Share na:

Iraq imemfukuza balozi wa Sweden katika hatua ya kupinga kitendo kilichopangwa cha kuichoma Qurani mjini Stockholm ambacho kilisababisha maelfu ya waandamanaji kutoka Iraq kushambulia na kuchoma moto ubalozi wa Sweden mjini Bagdad.

Taarifa ya serikali ya Iraq imesema Bagdad ilimwita balozi wake aliekuwa Sweden na kumrudisha Iraq.

Hata hivyo shirika la habari la serikali ya Iraq limeripoti kwamba Iraq ilisitisha kibali cha Balozi wa Sweden kufanya kazi kwenye ardhi yake.

Waandamanaji wanaopinga Uislamu nchini Sweden waliwasilisha maombi na kupewa ruhusa na polisi wa Sweden kuchoma Qurani nje ya ubalozi wa Iraq jana Alhamisi.

Katika tukio hilo, waandamanaji walipiga teke na kuharibu kwa kiasi fulani kitabu ambacho walisema ni Qurani lakini waliondoka eneo hilo baada ya saa moja bila kukichoma moto.

Waziri wa mambo ya nje wa Sweden Tobias Billstrom amesema wafanyakazi kwenye ubalozi wa Sweden mjini Bagdad wako salama lakini maafisa wa Iraq walishindwa kutekeleza wajibu wao wa kuulinda ubalozi.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya