ZINAZOVUMA:

Ummy Mwalimu awapa ‘tano’ Tanesco

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema uboreshwaji wa huduma za...

Share na:

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema uboreshaji wa huduma za afya nchini unategemea upatikanaji wa nishati ya umeme.

Akizungumza katika maonesho ya wiki ya Nishati yanayoendelea katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma Waziri Ummy amepongeza serikali na watendaji wote katika Sekta ya Nishati kwa kuendelea kuhakikisha watanzania wanapata nishati ya umeme ambayo pia inasaidia katika uboreshaji wa huduma za afya katika vituo vya afya kote nchini.

Waziri Ummy amesema hayo mara baada ya kutembelea banda la Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kwenye maonyesho ya Wiki ya Nishati inayoendelea kufanyika JIjini Dodoma katika viwanja vya Bunge.

“Upatikanaji wa umeme wa uhakika unasaidia pia katika kuboresha huduma za matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya hivyo kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa uharaka zaidi kwa kutumia vifaatiba.” amesema Waziri Ummy.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya