ZINAZOVUMA:

Hong Kong: Wafungwa wa kisiasa wanaweza wasitolewe mapema

Serikali ya Hong Kong imepitisha sheria mpya ya usalama wa...

Share na:

Kiongozi wa Hong Kong alisema siku ya jumanne kwamba wafungwa waliopatikana na hatia kwa uhalifu mkubwa wa usalama wa kitaifa hawataweza kuachiliwa mapema chini ya sheria mpya ya usalama wa kitaifa, kuashiria msimamo mgumu wa serikali dhidi ya wanaharakati wa kisiasa waliofungwa jela.

Mtendaji Mkuu wa Hong Kong John Lee alisema Sheria ya Kulinda Usalama wa Kitaifa inasema kwamba watu wanaopatikana na hatia ya kuhatarisha usalama wa taifa hawapaswi kusamehewa isipokuwa kamishna wa huduma za kurekebisha tabia (moja ya aina ya gereza) athibitishe kuwa hatua hiyo haitakuwa hatari kwa usalama wa taifa.

Hii inatumika pia kwa wafungwa ambao walipata hukumu kabla ya sheria mpya kuletwa Jumamosi iliyopita, Lee alisema.

Hapo awali, wafungwa wangeweza kupunguziwa vifungo vyao hadi theluthi moja kwa mwenendo mzuri chini ya sheria za magereza za jiji hilo, mradi tu wangekuwa wakitumikia vifungo kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Katika mkutano na waandishi wa habari wa kila wiki, Lee aliwataka wakaazi kutokiuka sheria.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya