ZINAZOVUMA:

Mkosoaji wa Putin ahamishiwa gereza lenye ulinzi mkali

Mkosoaji mkubwa wa Rais wa Urusi Vladimir Putin amehamishwa na...

Share na:

Mmoja kati ya wakosoaji wakubwa wa Urusi aliyekuwa gerezani amehamishiwa katika gereza lenye ulinzi mkali zaidi katika jimbo la Siberia na kuwekwa katika chumba kidogo cha adhabu.

Vladimir Kara-Murza Jr, mwenye umri wa miaka 42 alihukumiwa kwa uhaini kwa kulaani hadharani Urusi kuivamia Ukraine na kuhukumiwa kifungo cha miaka 25 gerezani.

Wakili wake Vadim Prokhorov amesema kupitia ujumbe wa Facebook, Jumapili, kwamba, mteja wake alihamishiwa katika gereza la IK-6, lenye ulinzi mkali katika mji wa Omsk jimboni Siberia.

Kara-Murza ambaye ni mwanahabari na mwanaharakati wa upinzani, aliwekwa jela Aprili 2022.

Mashitaka dhidi yake yalitokana na hotuba aliyoitoa katika baraza la wawakilishi la Arizona ambapo alitangaza kupinga uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya