ZINAZOVUMA:

Haiti: Majina ya Baraza la mpito yawasilishwa

Baada ya CARICOM kuingilia kati fujo za Haiti, leo wamefanikiwa...

Share na:

Viongozi wa nchi jirani wasema makundi yote na vyama vya siasa nchini Haiti, vimewasilisha majina ya wateule wao kwa ajili ya baraza la mpito la Rais. Baraza hilo lina jukumu la kuchagua waziri mkuu wa muda, ili kuondoa ombwe la kiungozi lililopo nchini Haiti pamoja na ghasia za magenge ya wahalifu.

Baraza la awali la wanachama tisa lilipunguzwa hadi wanachama wanane, baada ya chama cha Pitit Desalin, kinachoongozwa na seneta wa zamani, na mgombea urais Moïse Jean Charles kukataa nafasi hiyo.

Kundi llililoundwa Desemba tarehe 21 lililoshirikiana na Waziri Mkuu Ariel Henry lilikuwa mojawapo ya waliochukua hatua katika siku za mwisho likiwasilisha jina la mwakilishi wake juzi Jumatatu.

Rais wa Guyana Irfaan Ali alisema kuwa jumuiya ya kibiashara ya kikanda ya Caricom imekuwa ikikutana karibu kila siku kusaidia kuunda baraza hilo.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya