ZINAZOVUMA:

Ecuador yatangaza hali ya hatari kutokana na vurugu

Rais wa Ecuador atangaza hali ya hatari kwenye majimbo 7...

Share na:

Rais wa Ecuador Daniel Noboa siku ya Jumatano (Mei 22) alitoa taarifa mpya juu ya hali ya hatari, kwa majimbo 7 kati ya majimbo 24 ya nchi hiyo.

Na kusema kuwa kuna ongezeko la vifo kutokana na vurugu na uhalifu mwingine unaoendelea katika maeneo hayo.

Kwa mujibu wa amri hiyo iliyotiwa saini na Rais Noboa, hali ya hatari itadumu kwa siku 60 kwenye majimbo hayo.

Na majimbo yaliyoathirika ni Guayas, El Oro, Santa Elena, Manabi, Sucumbios, Orellana na Los Rios pamoja na eneo moja la jimbo la Azuay.

Serikali ilisema kwamba itawasilisha agizo hilo katika Mahakama ya Katiba, kwani katika hali ya hatari vikosi vya usalama vinaweza kuingia katika makazi ya watu au kunasa mawasiliano bila idhini.

Wakati Noboa akitangaza hali ya hatari siku ya Jumatano, Human Rights Watch (HRW) ilimsihi Rais Noboa kubatilisha tangazo lake la hali ya Hatari kutokana na vurugu za magenge yenye silaha.

Shirika la Human Rights Watch nchini Ecuador lilituma ujumbe huo kwa barua kwenda kwa Rais Noboa, na ksema kuwa juhudi za kutuliza ghasia bado hazijaleta matokeo chanya, ila inazidi hali ya usalama inazidi kuwa mbaya.

Pia iliongeza kuwa “matukio mengi ya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unafanywa na vikosi vya usalama vya nchi hiyo,” HRW iliongeza.

Barua hiyo iliongeza zaidi kwamba “watu wengi” wamezuiliwa tangu mwezi Januari ila “hawakuwahi kupelekwa mbele ya mwendesha mashtaka au hakimu,”  na kusema kuwa baadhi yao walipigwa na askari na polisi.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia aonekana kwenye hotuba yake kupitia mitandao wiki 3

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya