ZINAZOVUMA:

HAITI: Vifaa vya Mashirika ya kutoa misaada vyaibwa

Mashirika ya misaada nchini Haiti yalalamika kuibwa kwa vitu mbalimbali...

Share na:

Mashirika kadhaa ya serikali na yasiyo ya serikali yanayotoa misaada nchini Haiti yameripoti kuwa vitu mbalimbali vikiwemo vilivyotarajiwa kutolewa kama misaada imeporwa, ghasia za magenge ya wahalifu zikiibuka tena.

Makundi ya wahalifu nchini Haiti yamevamia taasisi muhimu na kufunga uwanja mkuu wa ndege wa kimataifa hivi karibuni.

Machafuko hayo yamewafanya raia wengi wa Haiti ukosefu wa chakula, na kukata tamaa.

UNICEF ilisema kuwa kontena lililojaa vifaa muhimu vya msaada limeporwa huku serikali ya Guatemala ikisema kuwa kituo cha ubalozi pia kiliibiwa.

Marekani ilipeleka ndege yenye vikosi vya kijeshi ili kuimarisha usalama katika Ubalozi wake, na kukanusha kwa vitendo uvumi kwamba maafisa wakuu wa serikali ya Marekani wanaweza kuondoka nchini humo.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,