ZINAZOVUMA:

Ebrahim Raisi afariki kwa ajali ya helikopta

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais...

Share na:

Vyombo vya habari nchini Iran vimetangaza kifo cha Rais wa nchi hiyo Ebrahim Raisi katika ajali ya helikopta, na mamlaka za nchi hiyo zikiwa hazijathibitisha taarifa hiyo ya vyombo vya habari.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Mehr, rais wa Jamhuri ya Iran, Ebrahim Raisi, alipata ajali wakati akiwa katika majukumu yake ya kitaifa na kwa ajili ya watu wa Iran.

Taarifa ya namna hii imeripotiwa pia na vyombo vingine vya habari vya ndani ya nchi ya Iran.

Ebrahim Raisi , Muhammad al Hashim (Imam wa Tabriz), Hossein Amir abdollahian (Waziri wa mambo ya nje) na Malik Rahmati Gavana wa jimbo la Azebaina mashariki (Kuanzia kulia)

Jumapili ya wiki iliyopita, moja ya shirika la habari la serikali ya Iran, lilitoa taarifa ya helikopta iliokuwa imembeba Raisi kupata ajali katika eneo la Jolfa, Mashariki mwa jimbo la Azerbaijan.

Taarifa hiyo ya iliendelea kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni hali mbaya ya hewa iliyokuwa katika eneo hilo.

Shirika la habari la serikali la IRNA katika taarifa yake pia lilieleza kuwa ajali hiyo ilitokea katika msitu Dizmar karibu na mji wa Varzeqan.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya