ZINAZOVUMA:

EACOP yagawa nyumba kama njugu

Uongozi wa mradi wa EACOP ukiwakilishwa na Wendy Brown umegawa...
Picha ya pamoja wakati wa ugawaji wa nyumba kwa walioathirika na mradi wa EACOP mkoani Tanga

Share na:

Meneja wa Mradi wa bomba la Mafuta (EACOP) Tanzania Wendy Brown, amegawa nyumba kwa baadhi ya wananchi waliothiriwa na mradi huo.

Mradi huo wa ujenzi wa bomba la mafuta unaanza Hoima nchini Uganda na kuishia Chongoleani.

Nyumba hizo zimejengwa katika maeneo ambapo, bomba hilo limepita na wananchi wamevunjiwa makazi.

Bomba hilo la EACOP limepita mikoa 8, wilaya 21 na vijiji zaidi ya 100 nchini Tanzania.

Nyumba hizo pia zitakuwa na tenki la lita 5000 la kuhifadhi maji, sola ya wati 200 na mfumo wake pamoja na betri ya 200Ah.

Mwaka jana walifanikiwa kugawa nyumba kwa wale walioathiriwa na kambi za wafanyakazi na yadi za bomba.

Kambi hizo na yadi kadhaa zipo wilayani Missenyi, Muleba, Bukombe, Nzega na Singida.

Huku bomba hilo likiwa limepita mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya