Spika wa Bunge la Jamuhurui ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson ametangaza kifo cha mbunge wa Kwahani Kisiwani Unguja Zanzibar, Mhe. Ahmed Yahya Abdulwakil ambacho kimetokea siku ya leo Jumatatu Aprili 8, 2024.
Dk, Tulia amebainisha hayo Bungeni Jijini Dodoma na kusema kuongezea kuwa Mbunge huyo amefariki ghafla kwa shinikizo la damu na mazishi ya marehemu yanatarajiwa kufanyika kesho Jumanne Aprili 9, 2024 Kijijini kwao Buyuni Zanzibar
Spika Tulia ameeleza kuwa kutokana na msiba huo kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa Bunge ya 173 hakutakuwa na kikao cha bunge ili kutoa nafasi kwa wabunge kushiriki msiba huo mpaka itakapofika Aprili 15, 2024.