ZINAZOVUMA:

Bolivia yaikana Israel na wengine kurudisha mabalozi

Bolivia, Chile na Colombia wavinja uhusiano wa kidiplomasia na Israel...
Mawaziri wa Bolivia wakitoa tamko la kuvunja uhusioano na Israel mbele ya Waandishi wa Habari
Mawaziri wa Bolivia wakitoa tamko la kuvunja uhusioano na Israel mbele ya Waandishi wa Habari. Waziri Ofisi ya Rais Bi Maria Nela Prada (Kushoto) na Naibu Waziri wa mambo ya nje Freddy Mamani (Kulia). Picha na AFP

Share na:

Nchi mbalimbali za Amerika ya Kusini zimekataa kuunga mkono mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza.

Bolivia imetoa tamko la kukata mahusiano ya kidiplomasia, na kushutumu kuwa Israel imepitiliza katika kuipiga Gaza.

Tamko hilo limetolewa na Naibu wa ziri wa Mambo ya Nje Fredy Mamani mbele ya waandishi wa Habari, na kusema kuwa mashambulzi ya Israelni fujo na hayana uwiano na yanayofanyika ukanda wa Gaza

Mbali na kuvunja uhusiano wa kidipomasia, pia nchi hiyo imetangaza kutuma msaada wa kibinadamu kwenda Gaza.

Hata hivyo Israel wanaona hakuna uhusiano wa kuvunjwa na Bolivia, na kuishutumu Bolivia kwa kukumbatia Iran ambao ni Magaidi.

Huku Hamas ikishindilia nyundo ya Bolivia kwa kuyataka mataifa ya kiarabu kujifunza kwa Bolivia.

Colombia na Chile ambazo ni jirani na Bolivia, zimeita mabalozi wake kama ishara ya kulaani mashambulizi dhidi ya Gaza na kuomba mashambulizi yasitishwe.

Tayari kna mataifa ya amerika ya kusini yanaunga mkono marekani na Israel, huku kuna mataifa kama Bolivia na majirani zake yakipinga mataifa hayo.

Hii si mara ya kwanza Bolivia kuvunja uhusiano wake na Israel, ilwahi kufanya hivyo mwkaa 2009 kupinga uvamizi wake dhidi ya Palestina.

Na uhusiano huo ulihuisha mwaka 2020, karibu miongo miwili tangu kuvunjika.

Pia nchi nyingne zilizotoa tamko la kutaka mapigano hayo yasitishwe ni Mexico na Brazil kwa Amerika ya Kusini.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya