ZINAZOVUMA:

Bakwata waja na mashindano ya hadithi za Mtume Muhammad (saw)

Mufti amesema mashindano hayo mapya hapa nchini yataendeshwa kwa mfumo...

Share na:

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakari Zubeir amesema Taasisi ya wanazuoni wa Africa tawi la Tanzania kwa kushirikiana na Baraza Kuu la waislam Tanzania (BAKWATA) wanakusudia kuanza kuandaa mashindano ya hadithi za Mtume Muhammad (SAW) kwa mwaka 2024.

Sheikh Abubakar ametoa taarifa hiyo hivi karibuni wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mipango ya Taasisi ya wanazuoni wa Africa ambaye yeye ni Mwenyekiti wake katika tawi la Tanzania.
Mufti amesema mashindano hayo mapya hapa nchini yataendeshwa kwa mfumo unaofanana na mashindano ya quran na kutakuwa na zawadi nono kwa watu watakaofanikiwa kushinda.

“Kwa miaka mingi kumekuwa na mashindano ya quran hapa nchini sasa wakati umefika wa kuandaa mashindano ya Hadithi za Mtume Muhammad (saw)”, alisema Sheikh Abubakar.

Aidha kuhusu mashindano ya quran kwa nchi zote za Africa, Mufti amesema mashindano hayo yataendelea kama kawaida, mashindano hayo ambayo fainali yake ilifanyika Tanzania kwa mwaka 2023, mwaka huu bado haijafahamika itafanyikia wapi.

Hivi karibuni Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir amefanya ziara za mfululizo, ameweza kwenda nchini Saudi Arabia ambako amekaa kwa siku nne na kufanya mambo makubwa ya kiislam.

Licha ya kuwa bado hajaweka wazi tija iliyopatikana katika ziara hiyo ya Makka na madina, Mufti aliweza kutumia nafasi hiyo kulombea taifa amani pamoja na kuiombea kheri serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan, kuwaombea dua watanzania lakini pia kutafuta fursa kwa waislam wa Tanzania.

Ziara ya Makka Mufti aliambatana na viongozi wa ngazi za juu wa Bakwata akiwemo Katibu wa Baraza la Ulamaa sheikh Hassan Chizenga, Mkurugenzi wa Hijja Sheikh Haidar Kambwili na Mkurugenzi wa Qur’ani Bakwata Sheikh Othman Kaporo.

Pia Mufti alitembelea mjini Rabbat Morocco. Kwenye ziara hii Mufti aliambatana na Katibu wake Sheikh Hemed Juma. Mufti alirejea Tanzania Februari 7, 2024 na kupata mapokezi makubwa kutoka kwa viongozi wake waandamizi.

Miongoni mwa watu maarufu waliompokea Mufti ni pamoja na Mkurugenzi wa Daawa Sheikh Aarif Tanzania, Afisa Itifaki msaidizi Bakwata Sheikh Rashid, Afisa utawala ofisi ya Mufti Alhaj Baguan na Afisa Itifaki Mwandamizi Alhaj Mkambako.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya