ZINAZOVUMA:

Ziara ya Mufti Morocco yaleta tija

Mufti ametoa wito kwa watanzania wenye sifa wakiwemo maimam,walimu wa...

Share na:

Imeandaliwa na Selemani Magali

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir amesema baraza lake linajivunia kuona linafanya harakati zenye kuinua elimu ya dini ya kiislam nchini na kwamba wataendelea kufanya hivyo katika kipindi chao chote cha utumishi kwani ndio kazi waliyotumwa na waislam.

Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, Mufti amesema harakati wanazozifanya ikiwamo kufanya ziara za nje ya nchi na kukutana na watdau mbalimbali zimeanza kuzaa matunda. Mufti ametaja matunda hayo kuwa ni pamoja na kupatikana kwa nafasi 200, ambapo tokea Baraza hilo kuundwakwe Zaidi ya miaka 50 iliyopita hakujawahi kutokea fursa kubwa kama hiyo.

Amesema siri kubwa ni kufanya kazi kwa Juhudi na maarifa na uwepo wa ushirikiano ndani ya Taasisi.
Hayo ameyasema wakati akieleza mafanikio yake ya ziara ya wiki moja aliyoifanya Mjini Rabbat Morocco ambako amefanikiwa kupewa nafasi 200 za maimamu wanaohitaji kuongeza ujuzi.

Vilevile, Mufti ametoa wito kwa watanzania wenye sifa wakiwemo maimam,walimu wa madrasa na makhatibu kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi 200 za masomo ya uimam zilizotolewa na chuo cha Takwiinul Aimma kilichopo Morocco.

Sheikh Abubakari ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mohammed VI Tawi la Tanzania amesema nafasi hizo zinawahusu jinsia zote wanaume na wanawake huku akiweka wazi kuwa kila mwaka wanakwenda watu 40.

Amesema wanatarajia kufanya usahili wa nafasi hizo mapema iwezekanavyo na kwamba yeyote anayeona anakidhi vigezo na masharti asipange kukosa kufika katika chumba cha mtihani unaotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Mohammed VI, Kinondoni Jijini Dar es salaam.

“Kabla ya Februari 29 tutakuwa tumeshafanya mtihani wa mchujo, tunahitaji watu ambao wanafahamu walau kwa uchache lugha ya kiarabu, mwenye uwezo wa kuhifadhi sura chache au msahafu mzima na vilevile wenye afya njema,” alisema.

Wenzetu wa Morocco wanaingia nchini Februari 29, baada ya hapo utafanyika mchujo wa mwisho kati ya machi 3-4 na watakaopiita katika mchujo huo ndio watakwenda Morocco kwa masomo.

Vilevile amesema, masomo wanayokwenda kusoma ni yanahusu uimamu na kwamba wakirejea watakuwa ni wabobevu katika sekta ya sharia pamoja na uimam.

“Wasomi hawa wakimaliza masomo yao wanatarajiwa kuja kuisaisaidia jamii yao katika ibada, pia watakuwa ni wataalam wa masuala ya sharia, kwa kweli ni masomo mengi watakwenda kupatiwa,” alisema
Alisema itakuwa ni aibu kwa waislam na taifa kwa ujumla kukosa watu wenye sifa zilizotajwa na kufanya nafasi hizo kupotea, haamini kama hali hiyo kama itatokea kwani wasomi wapo wengi.

Akieleza umuhimu wa nafasi hizo, Mufti Abubakar Zubeir amesema mataifa mengi yanatamani kuzipata na kwamba kwa ukanda wa Afrika Mashariki ni mara ya kwanza zinatolewa na wamependelewa watanzania.

“Ninatabia ya kufanya utafiti nikifika mahali, nilipokwenda Morocco niligundua wengi wanaosoma katika vyuo vyao ni kutoka mataifa ya Magharibi, huku Afrika Mashariki bado hawajafikiwa, nimeomba nafasi hizi kwa hiyo naomba zitumike vizuri,” aliongeza.

Pia, Mufti Abubakari Zubeir ambaye alikuwa akizungumza huku akionekana mwenye sura ya bashasha, amesema watakaobahatika kupata nafasi hizo watalipiwa kila kitu ikiwamo chakula, malazi, usafiri pamoja na kupatiwa dola 200 kama kalinda mfuko.

Toka kufika kwa Taasisi ya Mohamed VI wanazuoni wa Africa mwaka 2017, Bakwata imekuwa na ushirikiano mzuri na Taasisi hiyo ambapo miradi mbalimbali imefanikishwa kwa ufanisi.

Miongoni mwa miradi iliyoasisiwa na kuzinduliwa ni pamoja na Bakwata Online Academy. Mradi huo umenufaisha masheikh wengi wakiwemo wa Baraza na wasio wa Baraza.

Aidha matukio mengine ambayo yamefanyika kwa mafanikio na kuwa na mkono wa Mohammed VI wanazuoni wa Africa ni pamoja na uzinduzi wa kanzi data (data base) ya walimu wa madras na maimamu nchi nzima.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya