Mkuu wa wilaya ya Geita Hashimu Komba amesikitishwa na kuto kukamilika kwa ujenzi wa zahanati ya kata ya Kasamwa wilayani humo.
Ameeleza hayo katika mkutano wa hadhara uliyofanyika katika kata hiyo na kusema kuwa ujenzi huo ulianza toka mwaka 2019
Mh. Komba amesema hadi sasa shilingi Milioni 100 zimeshatumika kwenye ujenzi huo
Aidha amesema alipoanza kupitia taarifa mbalimbali ambazo amekuwa akipokea kupitia CSR ndipo alipo baini kuwa miradi hiyo imekuwa haikamiliki kwa wakati.
Hata hivyo Mkuu huyo wa wilaya ameagiza kukamilishwa kwa miradi yote ya CSR ikiwemo zahanati hiyo na kusema kuwa hajafurahishwa na kitendo hicho kwani kinapoteza uaminifu kwa wananchi.