ZINAZOVUMA:

ACT Wazalendo: Serikali ifanyeni Tume huru uchaguzi wa madiwani

Makamu Mwenyekiti Bara wa Chama cha ACT Wazalendo ameitaka serikali...

Share na:

Chama cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali kutekeleza ahadi yake ya kutunga sheria ya kuiwezesha Tume Huru ya Uchaguzi kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mwenyekiti Bara wa chama hicho, Isihaka Mchinjita kwenye mapokezi ya kumpongeza kwa kuchaguliwa na Mkutano Mkuu Taifa kuongoza chama kwa nafasi hiyo ya Makamu Mwenyekiti Bara.

shamra shamra hizo za kumpokea na kumpongeza zilifanyika jana katika ofisi za chama cha ACT Wazalendo zilizopo Lindi Mjini, Mkoani Lindi.

“Tarehe 2 Februari 2024 kwenye mchakato wa kutunga Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Serikali ilileta jedwali la maboresho ili kuipa dhamana Tume ya Taifa ya Uchaguzi kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi wa serikali za vijiji, mitaa na vitongoji kwa kuzingatia utaratibu utakaoainishwa na Sheria itakayotungwa na Bunge,” alisema Mchinjita.

“Kwa bahati mbaya, miswada ya Tume ya Uchaguzi na Uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani bado haijasainiwa na Rais kuwa sheria hadi sasa. Hatujui ni maboresho gani hasa yamepitishwa kuwa sheria. pili, hadi sasa, serikali haijaanza mchakato wa sheria iliyoahidiwa bungeni ya kuipa madaraka Tume ya Uchaguzi kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Tunaona dalili za serikali kupata kigugumizi katika kutekeleza ahadi yake”

“Ni muhimu Bunge lisimame kidete kuhakikisha maboresho yaliyofanyika Bungeni ya kuipa dhamana Tume ya Taifa ya Uchaguzi kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa yanazingatiwa. Ni muhimu mchakato wa kutunga sheria kwa suala hilo uanze sasa. ACT Wazalendo tumeshaiagiza Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Chama kuainisha vipaumbele vya ACT Wazalendo tunavyotaka kuwepo kwenye Sheria hiyo” alisisitiza Ndugu Isihaka Mchinjita.

Pia alisema kuwa akishirikiana na viongozi wenzake pamoja na Baraza Kivuli la Mawaziri la ACT Wazalendo, atahakikisha kuwa ACT Wazalendo kinaendelea kuwa chama kinara katika kuzisemea kero za wananchi wa Tanzani.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya