ZINAZOVUMA:

Zimbabwe yashutumiwa kuwaachia ‘wabakaji’

Wafungwa walioachiwa kwa msamaha wa raisi Zimbabwe wanajumuisha wabakaji wa...

Share na:

Muungano wa upinzani wa nchini Zimbabwe Citizens Coalition for Change (CCC) umedai kuwa zaidi ya wafungwa 4,000 walioachiwa huru kwa msamaha wa raisi wiki iliyopita wanajumuisha wabakaji wa watoto.

Raisi Emmerson Mnangagwa aliwasamehe wafungwa waliotoka katika magereza 47 ya nchi hiyo katika jaribio la kupunguza msongamano gerezani.

Mamlaka za magereza zilisema kwamba ubakaji ni miongoni mwa makosa ambayo hayakujumuishwa katika msamaha huo.

Hata hivyo video zilizosambazwa mtandaoni zilionyesha kile ambacho vyombo vya habari vya nchini humo vilisema ni wabakaji wakisherehekea uhuru wao huku baadhi yao wakisemekana kuwa wametumikia hukumu yao kwa chini ya mwaka mmoja.

CCC katika taarifa yake siku ya Jana Jumatano ilisema haikuwa sawa kuwaachilia wahalifu hatari na ambao hawajarekebishwa kujumuika tena na jamii.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya