ZINAZOVUMA:

Zimbabwe kupiga kura leo kuchagua Rais na wabunge

Raia wa Zimbabwe wamejitokeza kwa wingi kupiga kura kumchagua Raisi...

Share na:

Leo Jumatato Agosti 23, 2023 raia wa Zimbabwe wanatarajia kupiga kura za kumchagua Rais na wabunge wa nchi hiyo ikiwa ni uchaguzi wa pili wa kidemokrasia tangu mwaka 2017 ulivyofanyika kwa mara ya kwanza.

Katika kinyang’anyiro cha urais, Rais aliyepo madarakani Emmerson Mnangagwa (80) anawania tena kiti hicho huku akikumbana na upinzani mkubwa kutoka kwa Nelson Chamisa (45) anayeongoza chama cha Citizens Coalition for Change (CCC).

Wakati uchaguzi huo unaendelea chama cha upinzani CCC kimekuwa kikidai kuwa wanachama wake wanatafutwa na polisi ili wakamatwe huku pia wakilalamikia kuzuiwa vibali vya kufanya kampeni baadhi ya maeneo.

Vituo zaidi ya 12,300 vinatarajiwa kutumika leo katika zoezi hilo muhimu la kidemokrasia.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,