Klabu ya Yanga imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kutoka sare ya bila kufungana na klabu ya Rivers united ya nchini Nigeria katika mchezo uliochezwa siku ya jana tarehe 30 Aprili 2023.
Matokeo hayo yameifanya Yanga kuingia katika hatua hiyo baada ya kushinda mchezo wa awali uliochezwa nchini Nigeria na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri.
Baada ya Yanga kuweka historia hiyo sasa itakutana na timu ya Marumo Gallants ya Afrika kusini katika hatua ya nusu fainali ambapo mchezo wa kwanza utachezwa Tanzania Mei 10 2023 kabla ya kurudiana nchini Afrika kusini wiki moja baada.
Timu nyingne zilizofanikiwa kuingia katika hatua hiyo ya nusu fainali ya kombe la shirikisho ni Asec Mimosas pamoja na USM Alger.