Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kuwa umefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na kocha Mkuu wa timu ya wanawake Yanga princess, Sebastian Nkoma.
Yanga wamesema kuwa Kwa sasa benchi la ufundi la timu hiyo litakuwa chini ya kocha Fredy Mbuna mpaka msimu huu utakapomaliza.
Aidha hali ya timu hiyo Kwa msimu huu imekua ya kusuasua ikishikilia nafasi ya nne katika ligi kuu ya wanawake Tanzania.