ZINAZOVUMA:

Wizara ya Ardhi Zanzibar na Bara kushirikiana

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Tanzania Bara...

Share na:

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ya Tanzania Bara na Wizara ya Makaazi kutoka Zanzibar pamoja na Taasisi za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na lile la Zanzibar (ZHC) zimesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya ardhi na Nyumba.

Hatua hiyo ni moja ya utekelezaji wa mwongozo wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Ofisi ya Makamu wa Pili Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuhusu taasisi zisizo za muungano kukutana na kubadilishana uzoefu wa utendaji wa majukumu yao na namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali katika utekelezaji majukumu yao.

Utiaji saini makubaliano hayo ulifanywa na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anthony Sanga na upande wa Zanzibar ni Dk Mngereza Mzee Miraji huku NHC ikiwakilishwa na Mkurugenzi wake, Hamad Abdalah na ZHC ikiwakilishwa na Mwanaisha Ali Said.

Maeneo yanayokwenda kutekelezwa katika ushirikiano huo ni kukusanya, kuchakata na kubadilishana taarifa za ardhi baharini, kubadilishana uzoefu kwenye maendeleo na matumizi ya mifumo ya habari na teknolojia kwa sekta ya ardhi pamoja na kuandaa na kutekeleza sera, sheria na miongozo mbalimbali ya sekta ya ardhi.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya