ZINAZOVUMA:

WFP yahitaji msaada kukabiliana na njaa Afrika Magharibi

Shirika la Mpango wa chakula la umoja wa mataifa limeomba...

Share na:

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, limesema linahitaji ufadhili wa ziada ili kusaidia mamilioni ya watu wa Afrika Magharibi na Kati kuhimili njaa katika miezi kadhaa ijayo, ya msimu wa katikati ya mavuno.

Shirika hilo limesema kuwa uhaba wa fedha uliopo unamaanisha kwamba litaweza kusaidia takriban nusu ya watu milioni 11.6 waliolengwa, chini ya mpango wa dharura wa chakula, katika nchi, zikiwemo Burkina Faso, Nigeria na Chad, ambako wimbi la wakimbizi kutoka Sudan limekuwa shinikizo la ziada, kwa rasilimali chache zilizopo.

Migogoro na kupanda kwa bei za bidhaa kumechangia katika kuongezeka kwa uhaba wa chakula kwa miaka 10 katika maeneo ya Afrika Magharibi na Kati, kulingana na tathmini iliyofaywa mwezi Machi mwaka huu na shirika la usalama wa chakula wa kikanda, ‘Cadre Harmonise’.

Kiwango cha utapiamlo pia kimeongezeka, huku watoto milioni 16.5, wa umri wa chini ya miaka mitano, wakitarajiwa kuwa na utapiamlo wa hali ya juu mwaka huu, WFP ilisema.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya