ZINAZOVUMA:

Wenye degree na masters wakafundishe shule za msingi

Raisi wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amesema...

Share na:

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete amesema ili elimu ya Tanzania ipige hatua, ni wakati sasa wa Wizara ya Elimu nchini kuchukua hatua ya kupeleka walimu wenye shahada na uzamili katika shule za awali na msingi.

Jakaya ameyasema hayo leo Agosti 31, 2023 jijini Dar es Salaam katika hafla ya uchangiaji wa fedha za kuwezesha serikali kupata kiasi cha Dola za Marekani 50,000 za ‘GPE Multiplier Grant’.

Amesema, katika nchi zilizoendelea walimu wenye uzamili ndio wanaofundisha chekechea.

“Walimu wanaotoka vyuo vikuu wateremsheni kufundisha shule za msingi ndipo tutainua ubora wa elimu yetu”. Amesisitiza Kikwete

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya