ZINAZOVUMA:

Waziri wa Afya atoa neno video ya mhudumu Kivule

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema viongozi wameanza kufanyia kazi...

Share na:

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema tarari viongozi wa Mkoa wa Dar es salaam wameanza kufanyia kazi sakata la video inayosambaa kumuhusu mtumishi wa Afya akichambua, kusafisha na kuanika vifaa vya hospitali katika hospitali ya Kivule Mkoani Dar es Salaam.

Mapema leo kwenye mitandao ya kijamii imesambaa video ya mhudumu wa hospitali ya Kivule akisafisha kwa maji baridi ya bomba vifaa vilivyotumika kuhudumia wagonjwa vikiwemo vya upasuaji kinyume na taratibu za kiafya.

Waziri Ummy amesema kitendo hicho ni kinyume na taratibu na miongozo ya kanuni za udhibiti wa maambukizi (Infection Prevention and Control).

“Tayari vingozi wa mkoa wa Dar es salaam wanalifanyia kazi suala hili na watatoa Taarifa Rasmi”

Aidha Waziri Ummy amemshukuru mwananchi alierekodi na kuisambaza video hiyo na kuwataka wananchi kutoacha kuibua mambo kama hayo yanayotokea katika vituo vya kutoa huduma za Afya vya umma na binafsi.


Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya