ZINAZOVUMA:

Waziri Mkuu ataka agizo la JPM litekelezwe

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aiagiza mikoa ya kaskazini kutekeleza agizo...

Share na:

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Nishati kuhakikisha inaratibu utekelezaji wa agizo lililotolewa na Rais wa awamu ya tano, hayati John Magufuli la mikoa ya kanda ya kaskazini kuagiza mafuta kutoka ghala la Kampuni ya GBP lililopo jijini Tanga.

Alitoa agizo hilo jana, baada ya kufanya ziara ya siku moja jijini hapo na kutembelea ghala la kuhifadhia petroli, dizeli na mafuta ya taa.

Waziri Mkuu, alimkaribisha Mbunge wa Tanga, Ummy Mwalimu ambae alimlalamikia akisema kwamba licha ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na GBP wa kujenga ghala la kupokea, kuhifadhi na kusambaza mafuta nchini na nchi za ukanda wa Maziwa Makuu.

Bado wanunuzi wa mikoa ya kanda ya kaskazini wananunua mafuta yanayoingizwa kupitia Bandari ya Dar es Salaam.

“hili linatuumiza sana watu wa Tanga, licha ya Rais John Magufuli kutembelea ghala hili na kuagiza wanunuzi wa mikoa ya kanda ya kaskazini kununua mafuta kutoka Tanga kwa sababu ni karibu, utekelezaji wake unasuasua… Serikali inatakiwa kuingilia kati,” alisema Ummy, ambaye pia ni Waziri wa Afya.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya