ZINAZOVUMA:

Waziri ajiuzulu baada ya kuendesha gari akiwa amelewa

Waziri wa sheria nchini New Zealand amejiuzulu baada ya kusababisha...

Share na:

Waziri wa Sheria kutoka nchini New Zealand, Kiri Allan amejiuzulu mara moja baada ya kukabiliwa na mashtaka ya kuendesha gari akiwa amelewa na kusababisha ajali pamoja na kukataa kuongozana na polisi mara alipokamatwa.

Baada ya kukamatwa, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 39, alizuiliwa kituoni kwa saa nne kabla ya kuachiliwa, na anatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni kwa madai hayo.

Hakuna majeruhi walioripotiwa kutokana na ajali hiyo, ambayo ilitokea jijini Wellington.

Kulingana na Newshub, Bi Allan alisema katika taarifa yake kwamba amekuwa akipitia matatizo binafsi katika wiki za hivi karibuni yaliyopelekea kutokuwa katika hali yake ya kawaida, ambapo mwezi uliopita aliuthibitishia umma kuhusu kutengana na mwenzi wake na pia anakabiliwa na tuhuma za kushindwa kuwa na uhusiano mzuri na wafanyakazi wake.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya