ZINAZOVUMA:

WATU 21 WAFARIKI DUNIA KWA MAFURIKO MOROCCO

Share na:

Watu 21 wamefariki dunia na wengine 32 kujeruhiwa baada ya mafuriko yanayosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha jana Jumapili katika jimbo la pwani ya Atlantiki la Safi, lililoko kilomita 330 (maili 205) kusini mwa mji mkuu Rabat nchini Morocco.

Kwa mujibu wa taarifa ya mamlaka za Morocco iliyotolewa usiku wa kuamkia leo Jumatatu, Desemba 15, 2025 imeeleza wengi wa waliojeruhiwa tayari wamerejea nyumbani kutoka hospitali.

Mvua hiyo kubwa iliyonyesha kwa saa moja ilitosha kuharibu nyumba na maduka katika mji wa kale wa Safi, huku magari yakisombwa na maji na barabara nyingi zikikatika, huku juhudi za uokoaji zikiendelea.

Hali hii imezua hofu miongoni mwa wananchi wa Safi, huku mamlaka zikiwahaakikishia usalama na msaada kwa walioathirika.

Morocco kwa sasa inakabiliwa na mvua kubwa na theluji kwenye milima ya Atlas, hali inayojitokeza baada ya miaka saba ya ukame ambayo ilisababisha baadhi ya mabwawa ya maji kupungua kiasi kikubwa.

Mvua hizo zilizoanza kunyesha mwezi Novemba, zimeathiri nchi nyingine za kiarabu ikiwemo Saudi Arabia, Iran, yemen, Oman, Qatar, Bahrain, Umoja wa Falme za Kiarabu.

Endelea Kusoma