Msajili wa Vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amesema hadi sasa vyama vipya vya siasa 18 vimepeleka maombi ya kuomba usajili katika ofisi yake, huku akisisitiza bado wanaendelea na uhakiki wa vyama vilivyopo.
Hayo ameyasema leo Jumatatu Julai 17, 2023 jijini Dar es Salaam katika mkutano wa kikao kazi na viongozi wa vyama vya Siasa nchini ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kwenye uhakiki wa vyama hivyo.
“Nikweli kuna Vyama 18 vimeomba usajili lakini siwezi kuendelea na mchakato kabla ya kufanyika uhakiki wa vyama vilivyopo, na kikubwa wawe na subira zoezi la uhakiki linaanza Julai 20 Mwaka huu tukimaliza nafikiri tunaweza kuendelea na mchakato,” amesema.
Hatua hiyo imekuja ukiwa umebaki mwaka mmoja kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.