Zaidi ya watu saba wamejeruhiwa baada ya ‘lift’ waliokuwa wakiitumia kupata hitilafu katika jengo la Millennium Tower Makumbusho jijini Dar es salaam.
Lift hiyo iliporomoka kutoka ghorofa ya 10 mpaka chini huku ikiwa na watu hao ndani.
Jeshi la zimamoto na uokoaji baada ya kufika eneo la tukio wesema chanzo cha hitilafu ya ‘lift’ hiyo ni kuzidiwa uzito kwani ilitakiwa waingie watu nane lakini waliingia watu zaidi ya 10 kwa wakati mmoja.
Hata hivyo mafundi wa jengo hilo wamesema kuwa haujapita muda mrefu toka ‘lift’ hiyo ifanyiwe marekebisho.