ZINAZOVUMA:

Watoto 350,000 hukutwa na saratani kila mwaka

Shirika la Afya duniani WHO limesema kwa kila mwaka watoto...

Share na:

Shirika la Afya duniani WHO limesema kwa kila mwaka zaidi ya watoto 350,000 wanakutwa na saratani katika nchi masikini.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Tedros Ghebreyesus ambaye ameeleza kuwa 30% ya Watoto hao hupoteza Maisha kwa kukosa Matibabu

Amesema 25% tu ya Watoto wenye Saratani katika Nchi zenye kipato cha chini wanapata huduma sahihi za kiafya kulingana na matatizo yao wakati waliopo katika Nchi zenye Kipato cha Juu wakiwa na uhakika wa kupata Matibabu kwa 90%

Takwimu za WHO, zinaonesha Mwaka 2020 pekee, Wagonjwa wapya milioni 18.1 waligundulika duniani kote huku saratani ya matiti, mapafu, utumbo na tezi dume zikichangia idadi kubwa ya Wagonjwa kwa rika zote.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya