ZINAZOVUMA:

Watetezi wa haki za binadamu wataka Dkt Slaa na wenzake waachiwe

Mtandao wa watetezi wa Haki za kibinadamu pamoja na kituo...

Share na:

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA), Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) pamoja na Kituo cha Sheria za Haki za Binadamu (LHRC) kwa pamoja wamelaani vikali kukamatwa kwa Wakili Boniphace Mwabukusi pamoja na wanaharakati wa Haki za Binadamu; Dr Wilbroad Slaa, Mdude Nyagali na Peter Madeleka.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria za Haki za Binadamu (LHRC) Anna Henga, amesema kuwa watetezi wa Haki za Binadamu wana haki ya kutoa maoni kuhusu jambo lolote ikiwemo kuhusu maboresho ya mkataba wa bandari.

Aidha ameongeza kuwa watuhumiwa hao hawakutenda kosa la uhaini huku akitoa wito kwa Jeshi la Polisi na Ofisi ya Mwendesha Mashitaka kuwaachia huru kwa kuwa kukamatwa kwao kumetokana na misimamo yao juu ya mkataba kati ya Tanzania na Dubai.

Pia ameweka wazi kuwa kukamatwa kwa wana harakati hao ni kwenda kinyume na nia ya Rais kwani Rais Samia alisema wanaopinga kama wanahoja wajumuishwe kwenye tume ya mipango na sio kuwatishia.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya