ZINAZOVUMA:

Wasio na ajira kuongezewa posho Ujerumani

Serikali nchini Ujerumani imetangaza kuwaongezea posho wananchi wake ambao hawana...

Share na:

Ujerumani imetangaza kuwa kuanzia mwaka ujao posho za watu wasiokuwa na ajira zitaongezwa hadi euro 609 sawa na shilingi za Tanzania milioni 1.5 kwa mwezi kulinganisha na malipo ya sasa ya Euro 502.

Watu zaidi ya milioni tano watanufaika na ongezeko hilo la asilimia 12 ambalo serikali ya Ujerumani italitoa ili kuhakikisha watu hao waweze kujikimu kimaisha.

Serikali ya Ujerumani ilipitisha mageuzi makubwa katika mfumo wa ustawi wa jamii mwaka uliopita kwa manufaa ya watu ambao wamekaa muda mrefu bila ya ajira.

Mageuzi hayo pia yanalenga kutoa mafunzo ya kujipatia ujuzi kwa watu wasiokuwa na ajira. Posho kwa ajili ya watu wenye watoto pia zinatarajiwa kuongezwa.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya