Hali imekua mbaya nchini Afrika Kusini baada ya Mamlaka ya Huduma za Maji jijini Johannesburg kutoa tahadhari ikiwataka Wananchi kutumia Maji kidogo.
Tahadhari hiyo imetolewa ili kuzuia mfumo wa usambazaji maji usishindwe kabisa kusambaza kutokana na uhaba wa maji.
Wananchi wametakiwa kutumia vizuri kwa ustaarabu wanapokwenda kujisaidia pia watu waoshe Magari siku za mwisho wa wiki tu tena kwa ndoo moja ya Maji.
Aidha, Mamlaka imewataka wakazi wa Jiji hilo kuacha kujaza Mabwawa ya Kuogelea hadi uhaba wa Maji uishe, Kuepuka kumwagilia bustani na nyasi kwa Maji safi.
Uhaba wa Maji umeathiri maeneo mengine ikiwemo Taasisi muhimu zikiwemo Hospitali.