ZINAZOVUMA:

Wami Ruvu kusafisha mitaro morogoro Mjini

Bodi ya Maji ya Bonde la Wami Ruvu washirikiana na...

Share na:

Wananchi wametakiwa kuacha tabia ya kutupa taka ngumu katika mito na vyanzo vya maji Ili kuepuka uharibifu ambao unasababisha mito kujaa michanga na mifereji kuziba.

Akizungunza wakati wa zoezi la kufanya usafi katika mito kikundi Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu Mhandisi Pascal Joseph amesema katika mito ambayo inapita kwenye makazi ya watu kumekua na tabia ya utupaji taka hovyo na kusabisha uchafuzi wa mazingira.

Mhandisi Pascal amesema katika kuadhimishi wiki ya maji kuanzia Machi 16 huku kilele kikiwa ni Machi 22, wameanza kufanya usafi mto kikundi ,mitaro pamoja maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Morogoro.

Kwa Upande wake Mkuu wa Maabara ya ubora wa maji Mkoa Morogoro Sophia Patrick amesema uchafuzi wa Mazingira unachangia gharama za usafishaji maji na gharama za ankara (bili) kupanda.

Amesema suala la utunzaji vyanzo vya maji,mitaro na mazingira kwa ujumla ni jukumu la kila mtu hivyo kwa yeyote atakayekamatwa hatua Kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake .

Akizungumza katika zoezi hilo la usafi mmoja wa Wakazi wa Morogoro Abukabari Mwilima maarufu kama Mr Sounds amewashukuru Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu kwa kuwashirikisha wananchi katika zoezi hilo.

Mr Sounds amesema atakua balozi kwa wananchi katika kuhamasisha utunzaji vyanzo vya maji,mitaro pamoja mazingira kwa ujumla

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya