ZINAZOVUMA:

Walimu watishia kwenda kazini siku mbili pekee

Umoja wa walimu wa elimu ya juu nchini Nigeria umetoa...

Share na:

Umoja wa Walimu wa Elimu ya Juu (COEASU) unaojumuisha vyuo 252 nchini Nigeria umetoa tamko kuwa Wanachama wake wanatarajia kuanza kufanya kazi kwa muda wa siku mbili kwa wiki.

Hali hii inatokana na kupanda kwa gharama za maisha nchini humo na wamesema kwamba kama Serikali haitapunguza gharama za maisha basi waongezewe mishahara.

Walimu hao wanataka nyongeza ya mshahara kwa asilimia 200 ili waweze kuendana na gharama ya maisha ilivyo kwa sasa.

Hatua hiyo inakuja kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta ya Petroli baada ya ruzuku ya mafuta ya Serikali kuondolewa..

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,