ZINAZOVUMA:

Wahamiaji 65 kutoka Ethiopia wakamatwa Tanzania

Wahamiaji 65 kutoka nchini Ethiopia wamekamatwa na idara ya uhamiaji...

Share na:

Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania imewakamata wahamiaji haramu 65 raia wa Ethiopia ambao walikuwa wanasafirishwa kwenye gari la kubebea mafuta.

Wahamiaji hao walikuwa wanasafirishwa kutoka mkoani Mwanza kuelekea Tunduma ambapo Walikamatwa katika kizuizi kilichopo kijiji cha Kamsisi Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi.

Idara ya uhamiaji imesema kuwa pia watu 4 raia wa Tanzania walikamatwa akiwemo dereva wa gari hilo kwa kosa la kuwasaidia wahamiaji hao, Watu wote hao wanashikiliwa Kwa hatua zaidi za kisheria.

Mara kwa mara Tanzania hutumika kama njia ya kupita kwa wahamiaji haramu kutoka Eritrea na Ethiopia ambao wengi wao huelekea Afrika Kusini au Ulaya.

Kwa wale wanaoshindwa kufanikiwa safari yao huishia kukamatwa, wengine hutelekezwa na madereva wakiwa wamekufa au kuwa na hali mbaya kiafya.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM), linakadiria kuwa tangu mwaka 2014 karibu wahamiaji 50,000 wamekufa au kutoweka wakijaribu kufika nchi za Marekani au Ulaya.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya