ZINAZOVUMA:

Wafanyabiashara wazungumza bila uoga mbele ya Waziri Mkuu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali itatatua kero zote za...

Share na:

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewahakikishia Wafanyabiashara kote nchini kwamba Serikali ambayo inaongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imedhamiria kutatua kero na Changamoto mbalimbali zinazowakabili Wafanyabiashara kote nchini

Ametoa kauli hiyo Leo Jijini Dar es Salaaam wakati akizungumza na Wafanyabiashara waliokusanyika katika Viwanja vya mnazi mmoja kufuatia mgomo wa kutofungua Biashara zao katika Soko la Kariakoo.

Pia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewaruhusu Wafanyabiashara kuzungumza yale yanayowaumiza bila uoga na kuwaonya Viongozi kutowatisha Wafanyabiashara hao katika mkutano huo unaofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam

Aidha kwa upande mwingine pia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema Kuna sehemu wafanyabiashara wanaumizwa kutokana na mifumo, hivyo atalishughukia jambo hilo.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,