Baadhi ya Wafanyabiashara wa Mahindi kutoka Mikoa mbalimbali wamefunga mpaka wa Tanzania na Zambia upande wa Tunduma mkoani Songwe kwa zaidi ya masaa mawili, kwa kuegesha magari yao, wakishinikiza serikali ya Tanzania kukaa meza moja na serikali ya Zambia, ili iwapatiwe mahindi yao zaidi ya tani 1,200.
Wafanyabiashara hao wamesema kuwa mahindi hayo wamenunua kwa njia halali lakini yameshikiliwa kwa zaidi ya miezi mitano mpaka hivi sasa.
licha ya kuwa na vibali halali vya kununulia na kusafirishia mazao hayo kutoka nchini humo lakini wamezuiliwa kuyatoa mahindi hayo nje ya nchi ya Zambia.
Akielezea tukio hilo na hatua zilizochukuliwa na serikali,, Mkuu wa wilaya ya Momba Bw. Fakii Lulandala, amesema tayari serikali ya Zambia imewataka wafanyabiashara hao ambao wamenunua kihalali kuuza mahindi hayo ndani ya Zambia na si vinginevyo, huku akiwataka kuwa watulivu kwa kipindi hiki wakati suala hilo linatafutiwa ufumbuzi wa kudumu.