ZINAZOVUMA:

Waandamana kutaka majeshi ya kigeni kuondoka

Wananchi waandamana nchini Niger kupinga uwepo wa vikosi vya majeshi...

Share na:

Mamia ya waandamanaji wapinga uwepo wa majeshi ya kigeni nchini Niger, majeshi hayo yanajumuisha vikosi vya marekani vyenye kambi ya kijeshi kaskazini mwa nchi hiyo.

Waandamanaji hao wamekusanyika katikati ya mji mkuu wa Niamey, kuitikia wito wa mashirika ya kiraia yaliyo karibu na utawala wa kijeshi wa nchi hiyo.

Pia katika maandamano hayo wameonekana baadhi ya maafisa wa kijeshi nchini Niger, ikiwa ni ishara ya kuunga mkono harakati hizo za raia kutaka majeshi hayo ya kigeni yaondoke Niger.

Abdoulaziz Yaya, mmoja wa waandamanaji amesema: “tumetoa wito kwa wamarekani na vikosi vyote vya kigeni kutoka Niger, na uongozi wa jeshi umezingatia wasiwasi wetu”

Na kuongeza kuwa “tumekuja kuunga mkono na kuthibitisha uungaji mkono wetu kwa uongozi wa jeshi kuhusiana na uamuzi uliochukuliwa wa kutaka majeshi ya kigeni yaondoke”.

Maandamano hayo yamefanyika wakati taifa hilo la Afrika Magharibi likijiondoa katika ushirikiano wa karibu na Marekani katika juhudi za kukabiliana na ugaidi, na badala yake kuigeukia Russia kwa ajili ya masuala yake usalama.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya