ZINAZOVUMA:

Niger kusitisha Mkataba wa kijeshi na Marekani

Niger yavunja makubaliano yake na marekano baada ya marekano kuingiza...

Share na:

Utawala wa kijeshi nchini Niger umebatilisha mkataba wa kijeshi ambao uliruhusu kuwepo kwa wanajeshi na wafanyakazi wa kiraia kutoka Wizara ya Ulinzi ya Marekani katika ardhi yake, msemaji wa utawala Kanali Amadou Abdramane amesema Jumamosi.

Abdramane, akiongea kwenye televisheni katika taifa la Afrika Magharibi amesema ujumbe wa Marekani haukufuata taratibu za kidiplomasia na kwamba nchi yake haikujulishwa kuhusu waliomo ndani ya ujumbe wala tarehe ya kuwasili kwao au ajenda yao.

Ameongezea kwamba majadiliano yao yalihusu mpito wa sasa wa kijeshi nchini Niger, ushirikiano kati ya nchi hizo mbili na maamuzi ya Niger ya washirika katika mapambano dhidi ya wanamgambo wenye uhusiano na al-Qaida na kundi la Islamci State.

Tangu wakamate madaraka mwezi Julai mwaka 2023, utawala wa kijeshi wa Niger, kama walivyo watawala wa kijeshi katika nchi jirani za Mali na Burkina Faso, wameifukuza Ufaransa na majeshi mengine ya Ulaya, na kuigeukia Russia kwa msaada.

“Tunasikitika kuwa azma ya ujumbe wa Marekani ni kuwanyima kutunyima haki ya kuchagua washirika wetu na aina ya ushirika wenye uwezo wa kweli wa kusaidia katika mapambano dhidi ya ugaidi,” Abdramane amesema.

“Pia, serikali ya Niger inalaani vikali kwa nguvu tabia ya kujishusha chini inayoambatana na vitisho vya kulipiza kisasi kutoka kwa ujumbe wa Marekani kwa serikali ya Niger na watu,” ameongezea.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya