ZINAZOVUMA:

Wa kwanza ashtakiwa kushiriki mapenzi jinsia moja Uganda

Mtu wa kwanza ametuhumiwa tangu ipitishwe sheria mpya ya kudhibiti...

Share na:

Kijana mwenye umri wa miaka 20 nchini Uganda amekuwa raia wa kwanza kushtakiwa kwa vitendo viliyokithiri vya mahusiano ya mapenzi ya jinsia moja.

kosa hilo linaadhibiwa chini ya sheria mpya iliyopitishwa hivi karibuni nchini humo ikihusisha kifungo gerezani au kifo kwa atakaebainika akishiriki vitendo hivyo.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyoonekana na shirika la habari la Reuters, mshtakiwa alishtakiwa Agosti 18 kwa ulawiti uliokithiri baada ya kufanya ngono kinyume cha sheria na mwanamume mwenzake mwenye umri wa miaka 41.

Mahakama imesema kama kijana huyo atakutwa na hatia juu ya makosa hayo basi atachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria mpya ambayo imekua ikipingwa sana na watetezi wa haki pamoja na Jumuiya za kimataifa.

Sheria hiyo ndio ilipelekea Benki ya Dunia kutangaza kusitisha misaada nchini Uganda na kusema kuwa sheria walioiweka ni kinyume cha haki za binadamu, japo Uganda hajateteleka na imeendelea kusimamia sheria hiyo.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya