ZINAZOVUMA:

Vurugu za Maandamano Kenya: Watu 6 Wauawa na Risasi, Vifo Vyafikia 12

Katika maandamano ya Azimio la Umoja Kenya, watu sita wameuawa...

Share na:

Mpaka hivi sasa watu sita wameuawa baada ya kupigwa risasi katika maandamano ya Azimio la Umoja Kenya yaliyohusisha vurugu kati ya polisi na waandamanaji.

Kati ya waliouawa, watatu walipigwa risasi katika Mji wa Kitengela, mmoja huko Emali na wawili walipigwa eneo la Mlolongo kaunti ya Nairobi.

Takriban watu sita walifariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita kufuatia maandamano hayo na sasa idadi ya vifo kufikia 12.

Mtandao wa Nation, unaeleza kuwa waandamanaji huko Emali walichoma gari la polisi na kurusha mawe kwenye majengo ya benki moja, hali iliyosababisha shughuli za kiuchumi kusimama.

Waandamanaji hao wanaoipinga Serikali, wanadaiwa kujihusisha na uporaji pamoja na kuharibu miundombinu pembezoni mwa barabara eneo la Mlolongo, jijini Nairobi.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,