ZINAZOVUMA:

Vinicius alalamikia ubaguzi La Liga

Mchezaji wa Real Madrid Vinicius Junior ameilalamika ligi ya La...

Share na:

Mchezaji wa Real Madrid Vinicius Junior ameishutumu La Liga na kusema kuwa ni wabaguzi wa rangi baada ya kushambuliwa kwa maneno ya kibaguzi na mashabiki wa Valencia.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alipewa kadi nyekundu katika mchezo uliowakutanisha Real Madrid dhidi ya Valencia uliomalizika kwa Real Madrid kupoteza goli moja kwa bila.

Kocha wa Madrid pia amesema mwamuzi wa mchezo huo alitakiwa kusimamisha mechi kutokana na vitendo vya kibaguzi alivyofanyiwa Vini.

Baada ya mchezo Vinicius aliandika katika mitandao yake ya kijamii akiishutumu La Liga na kusema wanafumbia macho vitendo hivyo.

“Michuano ambayo hapo awali ilikuwa ya Ronaldinho, Ronaldo, Cristiano na Messi leo ni ya wabaguzi wa rangi,” aliandika Vinicius kwenye Instagram.

“Haikuwa mara ya kwanza, wala ya pili, wala ya tatu. Ubaguzi wa rangi ni jambo la kawaida kwenye La Liga. Wasimamizi wa mashindano hayo wanafikiri ni jambo la kawaida, Shirikisho na wapinzani pia wanaendekeza suala hili”.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya