ZINAZOVUMA:

Vikosi vya wanamgambo vimeichukua Darful

Mapigano yanayoendelea nchini Sudan mpaka sasa vikosi vya wanamgambo wa...

Share na:

Kikosi cha wanamgambo kinachopigana dhidi ya jeshi nchini Sudan kimechukua udhibiti wa mji wa Darfur Kusini huku kukiwa na ripoti zaidi za ukiukwaji wa haki za binadamu.

Mapigano kati ya Wanajeshi wa Rapid Support Forces (RSF) na jeshi la Sudan yamesababisha maelfu ya familia kukimbia makazi yao.

Hata hivyo kumekuwepo ripoti za wapiganaji wa RSF kupora au kuharibu majengo na masoko ya serikali.

Tangu vita vilipozuka katikati ya mwezi wa Aprili jumuiya zisizo za Kiarabu kote Darfur zimekuwa zikilengwa na RSF na wanamgambo washirika wa Kiarabu.

Mapigano makali yanaendelea katika mji mkuu, Khartoum, na katika maeneo mengine kadhaa huku juhudi za upatanishi za kikanda na kimataifa zikiendelea kumaliza mzozo huo.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya