ZINAZOVUMA:

Vijana 50 kulipiwa mahari na Al Hikma.

Taasisi ya Al Hikma Foundation imesema itawalipia mahari vijana 50...

Share na:

Taasisi ya dini ya Kiislamu ya Al- Hikma Foundation imetangaza kuwalipia mahari vijana 50 ambao wapo tayari kuoa.

Akizungumza katika mashindano ya 23 ya kimataifa ya kuhifadhi Qur’an ambayo yamefanyika Jana Jumapili Aprili 9, 2023 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Sheikh Nurdin Kishki ambaye ni mwenyekiti wa taasisi hiyo amesisitiza kuwa mahari hiyo haitawahusu wale wanaotaka kuongeza mke wa pili.

Kishki amesema sharti hilo limewekwa kwa asiye na mke kabisa ana haja ya kusaidiwa zaidi ya yule ambaye anataka kuongeza mke.

Amesema lengo lilikuwa kuozesha vijana 100 hivyo ametoa wito kwa yeyote mwenye kuweza kuunga mkono jambo hilo.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya